Jina la nchi limetoka kwa familia ya watawala, yaani familia ya aliyeianzisha, Chifu Ibn Saud wa Riyad. Yeye, baada ya kuondoka kwa jeshi la Waturuki Waosmani waliotawala Arabia kwa karne kadha, alishinda vita baina ya makabila ya Uarabuni ya kati akaweza kuvamia na kutawala maeneo ya Najd na Hejaz na mwaka 1932 alitangaza Ufalme wa Uarabuni wa Saudia