Mfano wa tofauti hizi ni maungano ya kifalme ya Uingereza na Hannover kati ya 1714 na 1837. Mtemi Georg Ludwig wa Hannover alirithi cheo cha mfalme wa Uingereza na watoto wa kiume wa familia waliendelea kuwa wakuu wa nchi zote mbili. Baada ya kifo cha mfalme William IV Uingereza ulimteua mpwa wake Victoria kuwa malkia mpya. Lakini sheria za Hannover hazikukubali mwanamke kama mtawala hivyo maungano ya kifalme kati ya nchi hizi mbili yalikwisha.