Hewa ina uzito wake. Kwenye uwiano wa bahari kila mita ya mjao huwa na uzito wa kilogramu 1,2041 kg. Kwa sababu angahewa inafikia kilomita mamia juu ya uso wa dunia kuna uzito wa tani 10 au kilogramu 10.000. Huu ni uzitoa tunaobeba kila siku lakini hatuusikii kwa sababu kwetu ni kawaida na tunaihitaji. Kama tungeondoka kutoka eropleni bila kinga katika kimo kikubwa sana kama juu ya kilomita 50 tungekufa haraka sana si tu kwa sababu huko hakuna hewa ya kutosha kwa kupumua lakini kwa sababu uhaba wa kanieneo ungesababisha damu yetu kuchemka.