TyDiQA1.0

The Typologically Different Question Answering Dataset

Predictions

Scores

Epifania

The Typologically Different Question Answering Dataset

Kwa kawaida Epifania inaeleweka kama sikukuu muhimu mojawapo ya Ukristo ambayo inahusiana na Noeli na inaadhimishwa kimapokeo tarehe 6 Januari. Lakini, kuanzia mwaka 1970, Kanisa la Kilatini limeruhusu Wakatoliki wa nchi ambapo tarehe hiyo si sikukuu ya taifa pia, waiadhimishe katika Jumapili ya kwanza baada ya Januari mosi, isije ikasahaulika. Upande wao, Makanisa ya Kiorthodoksi yanayofuata bado Kalenda ya Juliasi wanaiadhimisha siku ambayo katika nchi nyingi ni tarehe 19 Januari, kutokana na tofauti ya siku 13 kati ya kalenda hiyo na ile ya Gregori.