Alipata umashuhuri mwaka wa 2004 kufuatia kutolewa kwa wimbo wa "Locked Up", uliokuwa wa kwanza kutoka kwa albamu yake ya kwanza iliyoitwa, Trouble. Albamu yake ya pili, Konvicted, ilimwezesha kuteuliwa kushindania tuzo la Grammy kutokana na wimbo wa "Smack That". Yeye kufikia sasa ameanzisha kampuni mbili za kurekodi ambazo ni, Konvict Muzik na Kon Live Distribution. Yeye anajulikana kama mojawapo wa waimbaji waliofanikiwa na hodari zaidi wa mtindo wa R & B wa karne ya 21, apataye zaidi ya dola milioni 30 kwa mwaka . Haya ni kulingana na jarida la Forbes.